Hot story in Town: DAKTARI ALIYESABABISHA VIFO VYA WATU 13 INDIA MBARONI
#htmlcaption1 Go UP! Pure Javascript. No jQuery. No flash. #htmlcaption2 Stay Connected

Thursday, November 13, 2014

DAKTARI ALIYESABABISHA VIFO VYA WATU 13 INDIA MBARONI


Dk. RK Gupta aliyetiwa mbaroni.
DAKTARI anayehusishwa na tukio la vifo vya watu 13 katika kituo cha kutoa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji jimboni Chattisgarh nchini India, Dk. RK Gupta ametiwa mbaroni.



Baadhi ya akina mama waliofanyiwa upasuaji wakiwa hospitali.
Dk Gupta na msaidizi wake waliwafanyia upasuaji wananawake 83 katika kijiji cha Pendari ndani ya saa 3 Jumamosi iliyopita na kusababisha vifo 13 huku wengi wakiwa wamelazwa hospitali, 20 kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Rais wa India, Ram Avtar aliyempoteza mke wake aitwaye, Nem Bai akiomboleza na wanaye huko Bilaspur, Chattisgarh.


Ndugu na jamaa wakiomboleza kifo cha mama mmoja aliyefariki baada ya upasuaji huo.

Maandamano yamefanyika baada ya tukio hilo la vifo, huku serikali ya Jimbo la Chhattisgarh ikitoa amri ya kufanyika kwa uchunguzi.Serikali nchini humo inamtaka daktari mmoja kutoa huduma ya upasuaji kwa watu 35 tu kwa siku.

No comments:

Post a Comment