Hot story in Town: October 2014
#htmlcaption1 Go UP! Pure Javascript. No jQuery. No flash. #htmlcaption2 Stay Connected

Wednesday, October 22, 2014

TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA NNE WA MASWALA YA USALAMA MITANDAO

 KATIBU MKUU WIZARA YA SAYANSI MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA (PROF. PATRICK MAKUNGU) AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA WARSHA YA USALAMA MITANDAO AMBAPO TANZANIA IMEKUA MWENYEJI WAKE.
 MKURUGENZI MKUU WA COSTECH NCHINI (DR. HASSAN MSHINDA) AKITOA MANENO MACHACHE KATIKA UFUNGUZI WA WARHA HIYO.
 WASHIRIKI  KUTOKA KATIKA MATAIFA MBALI MBALI WAKIENDELEA NA WARSHA.
 WASHIRIKI  KUTOKA KATIKA MATAIFA MBALI MBALI WAKIENDELEA NA WARSHA.
 PICHA YA PAMOJA NJE YA UKUMBI WA MKUTANO

MHARIRI WA WASHINGTON POST AFARIKI

Mhariri wa zamani wa gazeti la Washington Post, Ben Bradlee enzi za uhai wake.

Mhariri wa zamani wa gazeti la Washington Post,  Ben Bradlee aliyeongoza uhariri wa kashfa ya Watergate miaka ya 70 na iliyosababisha Rais Richard Nixon kuachia ngazi amefariki akiwa na miaka 93.
Ben aliwahamasisha waandishi wawili wa habari Bob Woodward na Carl Bernstein kufuatilia kashfa hiyo ambayo Rais pia alijikuta akihusika.
Rais wa Marekani, Barack Obama akimvalisha medali ya Uhuru, Ben Bradlee.

Habari iliyochapishwa na gazeti hilo baadae ilionekana pia katika filamu na hivyo kumpa umaarufu mkubwa sana mwandishi huyu nguli.
Ben Bradlee hadi anakumbwa na mauti amekuwa ni miongoni mwa watu wanaohesabika kufanya kazi zenye tunu na hasa uadilifu aliouonyesha, Bwana alitoa na sasa amtwaa Amen.
Mwaka 1971, Bradlee (kulia), akiwa na Katharine Graham (kushoto).

Tuesday, October 21, 2014

MAN UNITED YAKWAA KISIKI

Mchezaji wa Manchester United, Marouane Fellaini (kushoto) akijiandaa kufunga bao lake la kwanza katika Ligi Kuu ya Uingereza dakika chache baada ya kuingia kutokea benchi akitoka Ander Herrera usiku wa kuamkia leo.
Saido Berahino akifunga bao la pili Westbromwich Albion kwa timu yale dakika ya 66 kipindi cha pili.
Blind's (katikati) akishangilia bao lake baada ya kusawazisha dakika tatu kabla ya mchezo kumalizika.
Kocha Mkuu wa Manchester Utd, Louis van Gaal.

Ligi kuu ya England imeendelea jana usiku ambapo Manchester United ilijikuta ikibanwa mbavu na kushindwa kufurukuta ugenini kwa Westbromwich Albion na kutoka sare ya mabao 2-2 licha kwamba ilitawala mchezo huo.

Mchezo huo wa pekee kwa ratiba ya ligi hiyo ulishuhudiwa Man United ikishindwa kupata walau ushindi wake wa kwanza nje ya uwanja wake wa nyumbani tangu timu hiyo iwe chini ya kocha Louis Van Gaal.

Ni bao la Daley Blind katika dakika za mwisho za mchezo ambalo limeiokoa Manchester United kuzama katika mpambano huo. Awali Stephane Sessegnon wa Westbrom aliitungua United kwa bao la mapema kabla ya Marouane Fellaini aliyeingia kipindi cha pili kusawazisha muda mfupi tu baada ya kuingia uwanjani.

Mshambuliaji kijana Saido Berahino aliipatia Westbrom goli la pili ambalo lilidumu hadi pale Blind aliposawazisha na kuinusuru United na kichapo katika mtanange huo uliochezeshwa na mwamuzi Mike Dean.

MIL.25 ZATUMIKA KILA MWAKA KUSAFISHA MAZINGIRA MBUGA YA MIKUMI


Wanachama wa Mtandao wa Habari za Kijamii Tanzania (Mhakita), wakifanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la Ujirani Mwema, wilayani Kilosa mkoani Morogoro, hivi juzi. Picha na Mpigapicha Wetu.
KIASI cha sh milioni 25 hutumika kila mwaka katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro kwa ajili ya shughuli za usafi wa mazingira na kuhudumia wanyama wanaogongwa katika barabara kuu iendayo Iringa na Morogoro inayopita katika hifadhi hiyo.

Kaimu mkuu wa hifadhi hiyo Dattomax Selanyika ,alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi habari waliotembelea katika hifadhi hiyo na kupata fulsa ya kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kupinga masuala ya ujangili kupitia mtandao wa habari za kijamii  Tanzania MHAKITA.

Alisema kati ya fedha hizo milioni 12.5 hutumika kwaajili ya uokotaji wa takataka zinazotupwa na wasafiri wanaotumia barabara hiyo.‘’ Usafi huo hufanywa na vibarua kuanzia eneo la Doma hadi Mikumi umbali wa kilomita 50, na shughuli hiyo hufanywa mara tatu kwa wiki’’ alisema Selanyika.
Aidha alisema katika maeneo yaliowekwa matuta ili magari yaweze kupunguza mwendo kutokana na kuwa ni vivuko vya wanyama pamegeuzwa ndio sehemu ya kutupa takataka kwa wasafiri hao.Alisema utupaji wa takataka katika hifadhi hiyo una madhara makubwa kwa wanyama kwani baadhi ya takataka husababisha wanyama kupoteza maisha wakizila.

Hata hivyo alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya madereva kwenda mwenzo kasi katika hifadhi, hiyo kinyume na sheria na kwamba kusababisha kuwagonga wanyama.Kwa upande wake mkuu wa idara ya ikologia wa hifadhi hiyo Crispin mwinuka alisema idadi ya wanyama wanaogongwa katika hifadhi hiyo wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika kipindi cha miaka 2009 hadi 2013 jumla ya wanyama 604 waligongwa katika barabara hiyo na kupoteza maisha.

Alisema mwaka 2012 wanyama waliogongwa walikuwa 111 huku mwaka 2014 walikuwa 132.Pia alisema katika kipindi hicho hicho jumla ya kilogramu 21,907.80 zilitupwa katika hifadhi hiyo na kusababisha hifadhi hiyo kuingia hasara kubwa katika kuokota taka hizo.Aliwataka wasafiri wanaotumia barabara hiyo kujenga tabia ya kuweka vifaa vya kuhifadhia takataka katika vyombo vya usafiri ili kuepusha tatizo hilo.

PISTORIOUS AFUNGWA MIAKA 5

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp enzi za uhai wake.

Hii ni baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp mwaka uliopita bila ya kukusudia.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa.

Upande wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake

Y-P WA TMK AFARIKI DUNIA


Wasanii wa Wanaume Family, kutoka kushoto, Dogo Aslay, Stiko na Yesaya Ambilikile YP (kulia) wakiwa katika pozi.
 Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile ‘ Y- P’ amefariki dunia usiku wa leo katika Hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua.
Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.

“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7 mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.

“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”