Alisema kati ya fedha hizo milioni 12.5 hutumika kwaajili ya uokotaji wa takataka zinazotupwa na wasafiri wanaotumia barabara hiyo.‘’ Usafi huo hufanywa na vibarua kuanzia eneo la Doma hadi Mikumi umbali wa kilomita 50, na shughuli hiyo hufanywa mara tatu kwa wiki’’ alisema Selanyika.
Aidha alisema katika maeneo yaliowekwa matuta ili magari yaweze kupunguza mwendo kutokana na kuwa ni vivuko vya wanyama pamegeuzwa ndio sehemu ya kutupa takataka kwa wasafiri hao.Alisema utupaji wa takataka katika hifadhi hiyo una madhara makubwa kwa wanyama kwani baadhi ya takataka husababisha wanyama kupoteza maisha wakizila.
Hata hivyo alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya madereva kwenda mwenzo kasi katika hifadhi, hiyo kinyume na sheria na kwamba kusababisha kuwagonga wanyama.Kwa upande wake mkuu wa idara ya ikologia wa hifadhi hiyo Crispin mwinuka alisema idadi ya wanyama wanaogongwa katika hifadhi hiyo wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika kipindi cha miaka 2009 hadi 2013 jumla ya wanyama 604 waligongwa katika barabara hiyo na kupoteza maisha.
Alisema mwaka 2012 wanyama waliogongwa walikuwa 111 huku mwaka 2014 walikuwa 132.Pia alisema katika kipindi hicho hicho jumla ya kilogramu 21,907.80 zilitupwa katika hifadhi hiyo na kusababisha hifadhi hiyo kuingia hasara kubwa katika kuokota taka hizo.Aliwataka wasafiri wanaotumia barabara hiyo kujenga tabia ya kuweka vifaa vya kuhifadhia takataka katika vyombo vya usafiri ili kuepusha tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment