Dakika chache baada ya kuondoka Bongo na kukwaa pipa, bebi mpya wa Diamond, Zari 'The Boss Lady' akiwa ndani ya ndege alionekana mwenye mawazo mazito katika picha alizotupia juzi kwenye fan page yake ya Face Book na Instagram ikisindikizwa na maneno: " miss you already TZ.....deep Mawazu....". Imedaiwa na wadau alikuwa anaamanisha kumkumbuka 'Sukari ya Warembo' zaidi kuliko TZ.....!
Thursday, November 13, 2014
BEBI MPYA WA DIAMOND AIKUMBUKA BONGO? AU?
Dakika chache baada ya kuondoka Bongo na kukwaa pipa, bebi mpya wa Diamond, Zari 'The Boss Lady' akiwa ndani ya ndege alionekana mwenye mawazo mazito katika picha alizotupia juzi kwenye fan page yake ya Face Book na Instagram ikisindikizwa na maneno: " miss you already TZ.....deep Mawazu....". Imedaiwa na wadau alikuwa anaamanisha kumkumbuka 'Sukari ya Warembo' zaidi kuliko TZ.....!
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KWENYE MAZISHI YA RAIS SATA WA ZAMBIA NOV 11, 2014
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima
za mwisho kwa mwili wa Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata
Ikulu mjini Lusaka Zambia Novemba 11,2014.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal wa kwanza
(kushoto) akiwa na Rais Mstaafu wa Zambia Mhe. Rupia Banda, Rais wa
Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta, Rais wa Msumbiji Mhe. Ermando Guebuza na
Kaimu Rais wa Zambia Dkt. Guy Scott kwenye Misa Maalum ya kuaga mwili wa
Rais Michael Sata iliyofanyika Novemba 11,2014 kwenye Uwanja wa Taifa
mjini Lusaka Zambia.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na
Katibu Mkuu wa Chama Tawala cha PF Mhe. A.B. Chikwanda kwenye Viwanja
vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa wakati mazishi ya
Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata yaliyofanyika Novemba
11,2014 kwenye uwanja wa Taifa mjini Lusaka Zambia.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais
mstaafu wa kwanza Zambia Dkt. Keneth Kaunda mara baada ya kumalizika
maziko ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja
vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika
Novemba 11,2014 mjini Lusaka Zambia.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akimfariji Rais
mstaafu wa Zambia Mhe. Ruphia Banda baada ya kumalizika mazishi ya Rais
wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye Viwanja vya Ubalozini
katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa yaliyofanyika Novemba 11,2014.
katikati Rais mstaafu wa kwanza wa Zambia Dkt. Keneth Kaunda.
.jpg)
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisaini kitabu
cha maombolezo ya Rais wa Zambia Marehemu Michael Chilufya Sata kwenye
Viwanja vya Ubalozini katika Makaburi ya Viongozi wa Kitaifa
yaliyofanyika Novemba 11,2014.
(Picha na OMR)
DAKTARI ALIYESABABISHA VIFO VYA WATU 13 INDIA MBARONI
Dk. RK Gupta aliyetiwa mbaroni.
DAKTARI anayehusishwa na tukio la vifo vya watu 13 katika kituo cha
kutoa huduma ya kuzuia uzazi kwa njia ya upasuaji jimboni Chattisgarh
nchini India, Dk. RK Gupta ametiwa mbaroni.
Baadhi ya akina mama waliofanyiwa upasuaji wakiwa hospitali.
Dk Gupta na msaidizi wake waliwafanyia upasuaji wananawake 83 katika
kijiji cha Pendari ndani ya saa 3 Jumamosi iliyopita na kusababisha vifo
13 huku wengi wakiwa wamelazwa hospitali, 20 kati yao wakiwa katika
hali mbaya.
Rais wa India, Ram Avtar aliyempoteza mke wake aitwaye, Nem Bai akiomboleza na wanaye huko Bilaspur, Chattisgarh.
Ndugu na jamaa wakiomboleza kifo cha mama mmoja aliyefariki baada ya upasuaji huo.
DIAMOND KUWABURUDISHA WATANZANIA PARTY YA UHURU WASHINGTON DC AKISINDIKIZWA NA 'TANZANIA ALL STARS NUNUA TICKET YAKO MAPEMA ZIKO LIMITED !!!!
TANZANIA ALL STARS -WIMBO MAALUMU WA MIAKA 53 YA UHURU
$100 (INCLUSIVE)
3 COURSE DINNER
BOTTLE OF CHAMPAGNE PER TABLE
LIVE ENTERTAINMENT
CELEB AFRICA TV RED CARPET COVERAGE
RE KNOWN PROFESSIONAL PHOTOGRAPHER
FREE PARKING
CASH BAR
SPONSORSHIP LEVELS STILL AVAILABLE
TICKET ZINAPATIKANA
SAFARI RESTAURANT
4306 GEORGIA AVENUE,NW
WASHINGTON,DC,20011
OR
ONLINE
OR
CALL
301-661-6207
240-764-9970
202-830-8970
*************************************
**************************************
NDG. JERRY SILAA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI SIMIYU
THE RICHEST PEOPLE IN AFRICA: MOHAMMED DEWJI NAMED YOUNGEST BILLIONAIRE IN AFRICA
24. Mohammed Dewji
Net Worth: $2 BILLION
Industry: Diversified
Country of Citizenship: Tanzania
Age: 39
Number of Jobs Created: 16,800
Mohammed Dewji has seen his net worth rise considerably over the past year as his MeTL group, a conglomerate in 11 countries with interests in trade, FMCG and manufacturing, undergoes significant expansion.
MWANAMUZIKI GEEZ MABOVU AFARIKI DUNIA
Kwa mujibu wa bwana Dennis ambaye alikuwa mtu wa karibu wa Geez Mabovu amethibitisha kuhusu kifo hicho na kusema rapa huyo aliondoka Dar kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya. Marehemu Geez Mabovu anatarajiwa kuzikwa leo Novemba 13, 2014.
Mwenyezi Mungu ailze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN
Wednesday, October 22, 2014
TANZANIA YAWA MWENYEJI WA MKUTANO MKUU WA NNE WA MASWALA YA USALAMA MITANDAO
KATIBU MKUU WIZARA YA
SAYANSI MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA (PROF. PATRICK MAKUNGU) AKIZUNGUMZA NA
WAANDISHI WA HABARI JUU YA WARSHA YA USALAMA MITANDAO AMBAPO TANZANIA
IMEKUA MWENYEJI WAKE.
MKURUGENZI MKUU WA COSTECH NCHINI (DR. HASSAN MSHINDA) AKITOA MANENO MACHACHE KATIKA UFUNGUZI WA WARHA HIYO.
WASHIRIKI KUTOKA KATIKA MATAIFA MBALI MBALI WAKIENDELEA NA WARSHA.
WASHIRIKI KUTOKA KATIKA MATAIFA MBALI MBALI WAKIENDELEA NA WARSHA.
PICHA YA PAMOJA NJE YA UKUMBI WA MKUTANO
MHARIRI WA WASHINGTON POST AFARIKI
Mhariri wa zamani wa gazeti la
Washington Post, Ben Bradlee aliyeongoza uhariri wa kashfa ya Watergate
miaka ya 70 na iliyosababisha Rais Richard Nixon kuachia ngazi
amefariki akiwa na miaka 93.
Ben aliwahamasisha waandishi wawili wa habari Bob Woodward na Carl
Bernstein kufuatilia kashfa hiyo ambayo Rais pia alijikuta akihusika.Ben Bradlee hadi anakumbwa na mauti amekuwa ni miongoni mwa watu wanaohesabika kufanya kazi zenye tunu na hasa uadilifu aliouonyesha, Bwana alitoa na sasa amtwaa Amen.
Tuesday, October 21, 2014
MAN UNITED YAKWAA KISIKI
Ligi kuu ya England imeendelea jana
usiku ambapo Manchester United ilijikuta ikibanwa mbavu na kushindwa
kufurukuta ugenini kwa Westbromwich Albion na kutoka sare ya mabao 2-2
licha kwamba ilitawala mchezo huo.
Ni bao la Daley Blind katika dakika za mwisho za mchezo ambalo limeiokoa Manchester United kuzama katika mpambano huo. Awali Stephane Sessegnon wa Westbrom aliitungua United kwa bao la mapema kabla ya Marouane Fellaini aliyeingia kipindi cha pili kusawazisha muda mfupi tu baada ya kuingia uwanjani.
Mshambuliaji kijana Saido Berahino aliipatia Westbrom goli la pili ambalo lilidumu hadi pale Blind aliposawazisha na kuinusuru United na kichapo katika mtanange huo uliochezeshwa na mwamuzi Mike Dean.
MIL.25 ZATUMIKA KILA MWAKA KUSAFISHA MAZINGIRA MBUGA YA MIKUMI
Alisema kati ya fedha hizo milioni 12.5 hutumika kwaajili ya uokotaji wa takataka zinazotupwa na wasafiri wanaotumia barabara hiyo.‘’ Usafi huo hufanywa na vibarua kuanzia eneo la Doma hadi Mikumi umbali wa kilomita 50, na shughuli hiyo hufanywa mara tatu kwa wiki’’ alisema Selanyika.
Aidha alisema katika maeneo yaliowekwa matuta ili magari yaweze kupunguza mwendo kutokana na kuwa ni vivuko vya wanyama pamegeuzwa ndio sehemu ya kutupa takataka kwa wasafiri hao.Alisema utupaji wa takataka katika hifadhi hiyo una madhara makubwa kwa wanyama kwani baadhi ya takataka husababisha wanyama kupoteza maisha wakizila.
Hata hivyo alisema kumekuwa na tabia ya baadhi ya madereva kwenda mwenzo kasi katika hifadhi, hiyo kinyume na sheria na kwamba kusababisha kuwagonga wanyama.Kwa upande wake mkuu wa idara ya ikologia wa hifadhi hiyo Crispin mwinuka alisema idadi ya wanyama wanaogongwa katika hifadhi hiyo wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo katika kipindi cha miaka 2009 hadi 2013 jumla ya wanyama 604 waligongwa katika barabara hiyo na kupoteza maisha.
Alisema mwaka 2012 wanyama waliogongwa walikuwa 111 huku mwaka 2014 walikuwa 132.Pia alisema katika kipindi hicho hicho jumla ya kilogramu 21,907.80 zilitupwa katika hifadhi hiyo na kusababisha hifadhi hiyo kuingia hasara kubwa katika kuokota taka hizo.Aliwataka wasafiri wanaotumia barabara hiyo kujenga tabia ya kuweka vifaa vya kuhifadhia takataka katika vyombo vya usafiri ili kuepusha tatizo hilo.
PISTORIOUS AFUNGWA MIAKA 5
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya
kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius akiwa na mpenzi wake Reeva Steenkamp enzi za uhai wake.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake
Y-P WA TMK AFARIKI DUNIA
Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.
“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7 mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.
“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”
Monday, September 29, 2014
WEMA SEPETU ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA
RAIS WA ZANZIBAR MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI CHUO CHA UDAKTARI ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman (katkati) wakisimama wakati wimbo
wa taifa ukipigwa katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari
Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za
Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja,(kushoto) Mkuu wa Kitivo cha Tiba DEAN
Ulpiano Perez na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Mohamed Saleh Jidawi.
Walimu
Madaktari Bingwa katika Chuo cha Madaktari Zanzibar kutoka Nchini CUBA
wakiwa katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar
yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya
Mbweni nje ya Mji wa Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Miongoni
mwa wahitimu wa Mafunzo ya Udaktari yaliyotolewa na Mataktari Bingwa
kutoka Nchini CUba wakila kiapo cha Utii wa kazi zao mbele ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa
mgeni rasmi katika mahfali ya kwanza yaliyofanyika leo katika viwanja
vya Chuo Mbweni nje ya Mji wa Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akitoa zawadi kwa Fatma Mrisho Haji akiwa ni miongoni mwa wanafunzi bora
waliopata zawadi katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari
Zanzibar yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za
Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja (katikati) Dk.Salhia Ali
Muhsin Mratibu wa Chuo.
Subscribe to:
Posts (Atom)