Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman (katkati) wakisimama wakati wimbo
wa taifa ukipigwa katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari
Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za
Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja,(kushoto) Mkuu wa Kitivo cha Tiba DEAN
Ulpiano Perez na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Mohamed Saleh Jidawi.
Walimu
Madaktari Bingwa katika Chuo cha Madaktari Zanzibar kutoka Nchini CUBA
wakiwa katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar
yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya
Mbweni nje ya Mji wa Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Miongoni
mwa wahitimu wa Mafunzo ya Udaktari yaliyotolewa na Mataktari Bingwa
kutoka Nchini CUba wakila kiapo cha Utii wa kazi zao mbele ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa
mgeni rasmi katika mahfali ya kwanza yaliyofanyika leo katika viwanja
vya Chuo Mbweni nje ya Mji wa Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akitoa zawadi kwa Fatma Mrisho Haji akiwa ni miongoni mwa wanafunzi bora
waliopata zawadi katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari
Zanzibar yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za
Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja (katikati) Dk.Salhia Ali
Muhsin Mratibu wa Chuo.
No comments:
Post a Comment