MH. PINDA AHUDHURI IBADA YA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MWAIPOPO WA DAYOSISI YA SUMBAWANGA
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakisalimiana na
Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga (kulia) katika Ibada ya
kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo
iliyofanyika kwenye kanisa kuu la kiinjili la Kilutheri la mjini
Sumbawanga Septemba 21, 2014. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakimkabidhi zawadi
Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo (wapili kushoto)
katika ibada ya kumweka wakfu Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu
la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga, Septemba 21, 2014. Kulia ni
mke wa Askofu huyo, Tunsume Mwaipopo na kushoto ni Askofu Israel
Mwakyolile wa Dayosisi ya Konde.
No comments:
Post a Comment