
Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Pwani Pauline Mrango akisoma
Hotuba ya makabidhiano ya mashine 28 za kufyatulia matofali kwa vikundi
vya vijana katika halmashauri zote za mkoa wa Pwani.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa pwani Pauline Mrango kwa
kutoa mashine 28 za kuwasaidia vijana.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria
makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika
la nyumba la Taifa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Pwani

Mashine 28 zitawasaidia vijana mkoa wa Pwani kuondokana na tatizo la
ajira, pili litasaidia sana katika utunzaji wa mazingira,zitasaidia
wananchi kujenga nyumba za kisasa na kwa bei nafuu.
Shirika la Nyumba la Taifa limetoa mashine hizo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 12 pamoja na mafunzo kwa vijana ya wiki mbili ambapo baada ya kumaliza mafunzo Shirika litatoa msaada wa shilingi laki tano kwa kila kikundi kama mtaji
( Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog)
No comments:
Post a Comment