

T.I
atafanya makamuzi pamoja na wasanii wengine mahiri wa hapa
nchini,watakao pangwa kushusha bonge la burudani kwa wale
watakaobahatika kupangwa kwenye orodha ya Oktoba 18, mwaka huu jijini Dar.
Nguli huyo mwenye albamu nane ambazo ni I'm Serious, Trap Muzik, Urban Legend, King, T.I. vs. T.I.P., Paper Trail, No Mercy na Trouble Man: Heavy Is the Head ambapo nyingi kati yake zimefanya vyema katika soko la muziki.
T.I ameshinda tuzo tatu za Grammy tangu aanze safari yake ya muziki.Baadhi ya singo kali alizoachia mkali huyo na kufanya vyema ni "Bring Em Out", "What You Know", "Big Shit Poppin' (Do It)", "Swagga Like Us" (FT Kanye West, Jay-Z na Lil Wayne), "Dead and Gone" (FT Justin Timberlake), "Ball" (FT Lil Wayne) na "No Mediocre" (FT Iggy Azalea).
No comments:
Post a Comment