Hot story in Town: SHEREHE YA MWAKA YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM‏
#htmlcaption1 Go UP! Pure Javascript. No jQuery. No flash. #htmlcaption2 Stay Connected

Monday, September 22, 2014

SHEREHE YA MWAKA YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF YAFANA JIJINI DAR ES SALAAM‏

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wa pensheni wa PPF wakati wa sherehe ya Mwaka iliyofanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Jijini Dar Es Salaam Mwishoni mwa wiki.
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akipokea cheti na zawadi kutoka Kwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka mara baada ya kutangazwa kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2013 kutoka Idara ya Mahusiano na Masoko ya Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sherehe ya mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar Es Salaam.
 Pichani Juu Ni baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara Mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PPF waliojipatia zawadi kwa kuwa wafanyakazi bora wa Mwaka 2013.
Wadau wakiserebuka Muziki mara baada ya wafanyakazi bora kupewa motisha na zawadi zao katika sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika Mwishoni mwa Wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Jijini Dar Es Salaam.
(Pichote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog)
 
 

No comments:

Post a Comment