Hot story in Town: September 2014
#htmlcaption1 Go UP! Pure Javascript. No jQuery. No flash. #htmlcaption2 Stay Connected

Monday, September 29, 2014

WEMA SEPETU ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akijiandaa kukata keki yake ya siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Kijitonyama.
Wema Isaac Sepetu akiongea na wageni wake (hawapo pichani) kabla ya kukata Ndafu.
Martin Kadinda (kushoto) akimuonesha Wema Sepetu kadi ya gari.
Gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa Wema Sepetu na mpenzi wake Diamond Platnumz.Gari aina ya BMW alilozawadiwa Wema Sepetu na meneja wake Martin Kadinda.

RAIS WA ZANZIBAR MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI CHUO CHA UDAKTARI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman (katkati) wakisimama wakati wimbo wa taifa ukipigwa katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja,(kushoto) Mkuu wa Kitivo cha Tiba DEAN Ulpiano Perez na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk.Mohamed Saleh Jidawi.
Walimu Madaktari Bingwa katika Chuo cha Madaktari Zanzibar kutoka Nchini CUBA wakiwa katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
 
Miongoni mwa wahitimu wa Mafunzo ya Udaktari yaliyotolewa na Mataktari Bingwa kutoka Nchini CUba wakila kiapo cha Utii wa kazi zao mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwa mgeni rasmi katika mahfali ya kwanza yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo Mbweni nje ya Mji wa Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa zawadi kwa Fatma Mrisho Haji akiwa ni miongoni mwa wanafunzi bora waliopata zawadi katika Mahfali ya Kwanza ya Chuo cha Madaktari Zanzibar yaliyofanyika leo katika viwanja vya Chuo cha Taaluma za Sayansi za Afya Mbweni nje ya Mji wa Unguja (katikati) Dk.Salhia Ali Muhsin Mratibu wa Chuo.

SERENGETI FIESTA YAFUNIKA MKOANI MBEYA

Msanii wa Bongo Fleva, Linex akitoa burudani usiku wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Barnaba Boy akifanya makamuzi jukwaani. Mr blue akifanya yake kwenye tamasha hilo
  Umati wa mashabiki katika Tamasha la Serengeti Fiesta usiku wa kuamkia leo ndani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.…

BONDIA WA KIKE MWAFRIKA ACHUKUA UBINGWA WA NGUMI ULAYA


  Bintou Yawa Schmill

Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill,mkazi wa Ujerumani siku ya ijumaa 26.September 2014 alifanikiwa kuchukua taji la ubingwa wa ngumi za kulipwa unaotambuliwa na IBF,Bondia Bintou alimpiga na kumshinda mpinzani wake bondia Mirjana Vujic kwa K.O katika raundi ya 3,. Pambano hilo lilionyeshwa Live katika TV channel ya euro sport na kutazamwa na maelfu ya watu wakishuhudia bondia wa kike mwafrika akirusha ngumi kali kuliko radi.
 
Bintou Schmill (30) aka The Voice ameshapigana mapambao ya kulipwa 9 na ameshinda 8 kwa K.O,Katika pambano la Ijumaa 26.September 2014 liliofanyika kwenye ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied,alifanikiwa kumpa wakati mgumu mpinzani wake kuanzia round ya kwanza hadi ilipofika raund 3 bondia Mirjana Vujickatika alipigwa kwa KO na Bintou Schmill aka "The Voice" kutangazwa ndie bingwa mpya wa uzito wa Welterweight barani ulaya na kuvikwa mkanda huo unatambuliwa na IBF.

Bintou Schmill aka 'The Voice' anaye fananishwa na Simba Jike (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou "The Voice" Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani !

Zaidi ya sh. Milioni 100 zapatikana katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund jijini dar

 Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah
Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,Ndg.
Ramadhan Madabida akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kuendesha harambee
hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar
es Salaam.Zaidi ya sh. Milioni 100 zilipatikana katika harambee hiyo.
Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust Fund,Bonnah Kaluwa akitoa hotuba
yake kwa wageni wa mbali mbali (hawapo pichani) waliohudhulia hafla ya
Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa Bonnah Education Trust Fund.
 Katibu wa Bonnah Education Trust Fund,Mary Muwasa akizungumza machache ikiwa
ni pamoja kuwatambulisha wadhamini mbali mbali waliojitolea ili
kufanikisha harambee hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli
ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rasmi katika hafla ya Chakula cha jioni cha kuchangia Mfuko wa
Bonnah Education Trust Fund,Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Dar es Salaam,Ndg.
Ramadhan Madabida (kushoto) akipokea mfano wa hundi ya Dola za Marekani
Elfu 8 kutoka kwa Mwenyekiti wa GCUT Group Tanzania,Lucy Jeremiar
Gilya.Katikati ni Mwenyekiti Mwanzilishi wa Bonnah Education Trust
Fund,Bonnah Kaluwa.

DIAMOND AMZAWADIA WEMA MURANO

Gari aina ya Nissani Murano alilozawadiwa Wema Sepetu na mpenzi wake Diamond Platnumz.

STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amemzawadia gari aina ya Nissan Murano mpenzi wake Wema Isaac Sepetu katika bethidei yake jana.

Kupitia akaunti yake ya Facebook na Instagram, Diamond ameweka picha ya gari aina ya Nissan Murano aliyompatia Wema na kuandika kuwa alitamani ampe mpenzi wake huyo vitu vingi, pengine ingesaidia kueleza ni kiasi gani anapenda amuone akifurahi kwenye siku yake ya kuzaliwa japo hana uwezo huo.

Diamond aliongeza kuwa, tafadhali pokea hiki nilichojaliwa na siku zote tambua kwamba Platnumz wako anakupenda sana! Nakutakia bethidei njema bebi. Alimalizia Diamond kupitia Facebook.
Kupitia ukaunti yake ya Instagram, Diamond ameandika hivi:



Wednesday, September 24, 2014

RASIMU ILIYOPENDEKEZWA BUNGE MAALUMU LA KATIBA‏


Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta.

BOFYA HAPA KUSOMA :::>  RASIMU YA KATIBA INAYOPENDEKEZWA

WANAFUNZI WA CHEKECHEA TUNDURU WASOMEA CHINI YA MTI

Wanafunzi wakiendelea na masomo wakiwa na mwalimu wao.

WANAFUNZI wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wanasomea chini ya mti kutokana na darasa hilo kuendeshwa bila ya kuwa na chumba maalum kwa ajili ya kusomea wanafunzi hao.

Hali hiyo imebainika baada ya mwandishi wa habari hizi kuitembelea shule hiyo hivi karibuni na kuwakuta wanafunzi wakiwa wamekaa chini huku wakiendelea na masomo hayo nje chini ya mti ulio na kivuli cha kuwahifadhi wakati wa jua kali.

Akizungumza shuleni hapo Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nakayaya, Christina Mhowera alisema watoto hao wamelazimika kusomea nje baada ya huduma ya elimu hiyo kuanzishwa shuleni hapo bila ya kuwa na jengo maalum kwa wanafunzi wa awali.

Alisema awali wanafunzi hao walikuwa wakisomea kwenye gofu (jengo mbovu) lililokuwa jirani na shule, lakini walilazimika kuondolewa baada ya jengo hilo kutwaliwa kwa matumizi mengine. Aliongeza kuwa baada ya hapo walihamishiwa kwenye nyumba ya mwalimu kabla ya kukamilika lakini waliondolewa tena na kuanza kusomea nje (chini ya mti) hadi sasa.

Alisema darasa hilo lenye jumla ya wanafunzi 92 linaendeshwa bila ya kuwa na chumba cha darasa maalum wala madawati kutokana na shule hiyo kukabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa hadi hapo watakapopata darasa maalum kwa ajili ya wanafunzi hao.

Kwa upande wake mwalimu wa darasa hilo, Teckla Milanzi alisema mbali na darasa hilo kutokuwa na chumba cha darasa, linakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo ya uhaba wa vitendea kazi kama vitabu na vyenzo zingine za kufundishia na hakuna bajeti yoyote inayotumwa kuliwezesha darasa hilo.

Aidha uchunguzi uliofanywa katika shule nyingine tatu za Wilaya ya Tunduru, yaani Shule ya Msingi Nanjoka, Majengo na Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko kuangalia mazingira ya utoaji elimu ya awali katika shule hizo umebainisha kukabiliwa na changamoto nyingi hali ambayo inahatarisha msingi wa elimu kwa wanafunzi.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nanjoka, Batadhari Mkwela alisema licha ya usajili wa wanafunzi wa awali kuongezeka kila mwaka kumekuwa hakuna bajeti ya kuendesha elimu hiyo.
“…Darasa la awali linahitaji vitendea kazi lakini havipo, hatuna vifaa kama vitabu vya kutosha, vyenzo za kufundishia, hakuna bajeti hata ya vifaa hivi toka Serikalini, hatuna madawati maalum kwa ajili ya wanafunzi wa awali,” alisema Mkwela.

Akizungumzia hali hiyo, Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Tunduru, Abdul Kazembe alisema vyumba vya madarasa ni changamoto kubwa eneo hilo licha ya msisitizo kuendelea kutolewa wa kila shule ya msingi kuwa na darasa la awali. Alisema mwaka 2013/14 halmashauri ya wilaya hiyo ilihitaji zaidi ya milioni 366.7 lakini ililetewa zaidi ya milioni 196.5 fedha ambayo ni karibia nusu tu ya kiasi kilichopitishwa kwenye bajeti hiyo.

“…Kwa hiyo unaweza kuona kwamba ni ngumu kuigawa fedha hii katika matumizi maana kwanza haitoshi na pili hata kilichotegemewa kuja ni pungufu zaidi tena sana, sasa sijui unaweza kugawa kila shule ipate shilingi ngapi…kwani haitoshelezi,” Abdul Kazembe.

Akifafanua zaidi Kaimu Ofisa Elimu huyo alisema miundombinu ya madarasa ni changamoto kubwa, kwani mwaka 2013 idadi ya mahitaji ya madarasa kwa wilaya nzima ilikuwa ni 1,715 lakini madarasa yaliopo ni 900 na kitu huku mengine yakiwa ni ya muda mrefu na yanaelekea kuchakaa.

MAMA SALMA KIKWETE AHUTUBIA MKUTANO WA ELIMU NA AFYA KWA VIJANA DUNIANI ULIOANDALIWA NA TAASISI YA MAMA SARAH BROWN

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa :’Getting serious about Results: The Grand Convergence of Education and Health’ ambao ulizungumzia mambo ya elimu na afya kwa vijana hapa duniani. Mkutano huo ilifanyika huko New York tarehe 23.9.2014.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Bwana Gordon Brown kabla ya kuanza
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Sarah Brown, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza na Mwenyekiti Mtendaji wa Global Business Coalition for Education muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa ‘Getting Serious About Results: The Grand Convergence of Education and Health” ulioandaliwa na Taasisi ya Mama Sarah Brown kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa. Mkutano huo umefanyika huko New York tarehe 23.9.2014. 

MWANAMUZIKI RAPPA MAHIRI KUTOKA NCHINI MAREKANI T.I KUSAMBAZA UPENDO NDANI YA TAMASHA LA FIESTA OKTOBA 18,2014 JIJINI DAR

Mmojawa Marappa mahiri kutoka nchini  Marekani atambulikae kwa jina la Clifford Joseph Harris,'T.I' ni mmoja wa wanamuziki watakaoangusha bonge la shoo la kusambaza upendo kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake,katika onesho la Fiesta 2014 linalotarajiwa kufanyika ndani ya Viwanja vya Leaders Club   jijini Dar es Salaam Oktoba 18.

T.I
atafanya makamuzi pamoja na wasanii wengine mahiri wa hapa
nchini,watakao pangwa kushusha bonge la burudani kwa wale
watakaobahatika kupangwa kwenye orodha ya Oktoba 18, mwaka huu jijini Dar.

Nguli huyo mwenye albamu nane ambazo ni I'm Serious, Trap Muzik, Urban Legend, King, T.I. vs. T.I.P., Paper Trail, No Mercy na Trouble Man: Heavy Is the Head ambapo nyingi kati yake zimefanya vyema katika soko la muziki.

 T.I ameshinda tuzo tatu za Grammy tangu aanze safari yake ya muziki.Baadhi ya singo kali alizoachia mkali huyo na kufanya vyema ni "Bring Em Out", "What You Know", "Big Shit Poppin' (Do It)", "Swagga Like Us" (FT Kanye West, Jay-Z na Lil Wayne), "Dead and Gone" (FT Justin Timberlake), "Ball" (FT Lil Wayne) na "No Mediocre" (FT Iggy Azalea).

WEMA AFANYA KUFURU UZINDUZI WA YAMOTO BAND

 Aslay akimwagiwa minoti na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.
Aslay akifurahiya minoti aliyomwagiwa na Beutiful Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’.
Wema Sepetu ‘Madam’ akiwa na marafiki zake.
Tukio hilo limetokea ndani ya ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem na kuweka historia kwa Wema kuwa staa wa kwanza ‘kumwaga’ fedha wakati wa uzinduzi wa bendi ya Yamoto.

MAMBO YALIVYOANZA
Awali, wakati bendi ya Yamoto ilipokuwa ikitumbuiza, ulifika wakati kiongozi wa bendi hiyo, Said Fella alitambulisha uwepo wa Wema kwa kudai amemuwakilisha bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivyo apande jukwaani na kusema chochote lakini mrembo huyo akasema kilichompeleka ukumbini hapo ni uzinduzi wa Yamoto Band.

“Jamani nimekuja hapa kwenye uzinduzi wa Bendi ya Yamoto na siyo kumuwakilisha Diamond, ya huku hayamuhusu kabisa sasa semeni niwaimbie wimbo gani,” alisikika Wema Sepetu na kuanza kuimba wimbo wa Niseme ambao mashabiki waliupendekeza.

AMWAGA FEDHA
Mrembo huyo asiyechuja tangu alipotwaa taji la u-miss Tanzania (2006), akiwa na wapambe wake, baada ya kuimba kidogo, alichukua pochi yake na kuanza kummwagia fedha mfululizo Dogo Aslay huku akiwa anamzunguka kwa kucheza.

ASLAY APAGAWA
Kwa fedha hizo zilizokadiriwa kuzidi milioni moja alizotunzwa Aslay, ilifika wakati dogo huyo akawa anaziangalia tu kama bubu na kupigwa butwaa huku akiishia kuzitazama bila kuimba chochote.

BAUNSA AMZUIA WEMA
Katika hali iliyowashangaza wengi, baunsa mmoja aliyekuwa akimlinda Wema alimzuia staa huyo kuendelea kutoa fedha zaidi akidai zimetosha ndipo akaacha na kushuka jukwaani.

 Wakati zoezi hilo likiendelea, kuna baadhi ya mashabiki waliibua minong’ono wakihoji kwa nini atunzwe Aslay peke yake wakati bendi hiyo ina wakali wengine watatu, Malomboso, Enock na Beka?

“Mbona kama anampendelea Aslay tu  wengine hawatunzi ona hela zote ameshikilia yeye tu kweli, inaonekana anamzimia sana Aslay, si bure, haikatazwi lakini,” alihoji shabiki mmoja aliyekuwa akifuatilia shoo hiyo.

Wema ameonekana kuja juu kwa sasa kifedha, wiki iliyopita alifanya tukio kama hilo katika Ukumbi wa Thai Village Masaki kwa kumtunza ‘pesa ndefu’ mwanamuziki wa Bendi ya Skylight, Sam Mapenzi huku ikidaiwa ni mwendelezo wa kampeni ya kumziba mdomo aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ambaye inadaiwa kwa sasa yuko ‘vizuri’ kifedha.

Picha kwa hisani ya Global

MATATIZO YA UGONJWA WA MOYO WA KUZALIWA (CONGENITAL HEART DISEASE)


Leo tutajadili baadhi ya matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo, yaani Congenital Heart Disease.

Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo ni mengi, kuanzia yale yanayosababishwa na matatizo madogomadogo ambayo kwa kawaida huwa hayaonyeshi dalili au kuathiri maisha ya kawaida ya mtu, hadi yale makubwa yanayohitaji kutibiwa kwa haraka.

Mara nyingi matatizo ya moyo ya kuzaliwa ni yale yanayozuia mtiririko wa damu katika moyo au kwenye mishipa ya damu, au kusababisha damu ipite njia nyingine isiyokuwa ya kawaida kwenye moyo.

Matatizo mengine ya moyo ya kuzaliwa lakini yasiyotokea sana ni pale baadhi ya chemba za moyo zinapokosekana au badala ya kuwepo chemba mbili mtoto huzaliwa na chemba moja ya ventricle au wakati mwingine upande wa kulia au wa kushoto wa moyo huwa haujaumbika kwa ukamilifu hali ambayo kitaalamu huitwa hypoplastic heart.

Miongoni mwa sababu zinazosababisha watoto kuzaliwa na matatizo ya moyo ni pamoja na mmoja kati ya wazazi kuwa na tatizo la moyo la kuzaliwa. Iwapo mama alikuwa na tatizo la moyo la kuzaliwa kuna uwezekano wa asilimia 2.5 hadi 18 wa kuzaa mtoto mwenye tatizo la moyo pia. Iwapo baba alikuwa na tatizo la moyo la kuzaliwa uwezekano wa kuzaliwa mtoto mwenye tatizo la moyo ni kuanzia asilimia 1.5 hadi 3.

Si kawaida mtoto zaidi ya mmoja kuzaliwa na tatizo la moyo katika familia moja. Kuna uwezekano  mtoto aliyeko tumboni wakati moyo unapoumbwa akapatwa na maambukizi ya maradhi kama vile  rubella, au kuathiriwa na dawa anazotumia mama wakati wa ujauzito au sumu kama vile lithium na hata pombe.

Yote hayo yanaweza kusababisha mtoto azaliwe na matatizo ya moyo. Lakini pia baadhi ya matatizo ya jenetiki huambatana na matatizo kadhaa ya moyo ya kuzaliwa. Matatizo hayo ya jenetiki kitaalamu huitwa Down’s Syndrome, Digeorge syndrome na Turners   Syndrome.

Jambo lingine linaloweza kusababisha mtoto azaliwe na matatizo ya moyo ni pale mama anapokuwa na tatizo la kijenetiki linalojulikana kama Phenylketonuria (PKU). Hali hiyo hutokea wakati mwili unaposhindwa kuyeyusha sehemu ya protini inayoitwa phenylalanine (Phe).

Phenylalanine kwa kawaida hupatikana katika kila chakula lakini kiwango chake kinapokuwa juu mwilini huweza kuharibu ubongo na kusababisha mtindio wa ubongo. Baadhi ya wajawazito hupata tatizo hilo ambalo huzidisha uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya moyo na ya ubongo pia.

Itaendelea wiki ijayo.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ZIARANI HANDENI,AZUNGUMZA NA WANANCHI NA KUKAGUA MAENDELEO YA MIRADI MBALIMBALI



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kwaluguru wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara katika shule ya sekondari Kwaluguru wilayani Handeni.

































Wananchi wa kata ya Kwaluguru wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana  wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Kwaluguru ambapo vyumba 83 vya maabara vinajengwa wilayani Handeni.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Kweinjugo kata ya Kwaluguru wilaya ya Handeni


Monday, September 22, 2014

BBA: MEET HOTSHOTS LAVEDA, KACEY MOORE AND JJ

Laveda - Tanzania
Age: 23

Bachelor of Arts & Social Sciences graduate Laveda was born in Dar Es Salaam. She’s single and describes herself as ‘eccentric, loving, caring, simple and fun’.
 Laveda is the eldest of three children and she has a younger brother and sister. She says her mom is her role model, because she has moulded her over the years and inspired her in different ways ‘through the struggles and joy of life’.

Laveda says her favourite foods are pasta and minced meat, and prawns. She loves to read John Grisham novels and enjoys the music of Shakira, D’Banj, Miriam Makeba, P.Square, Rihanna, Beyonce, Tiwo Savage, Yvonne Chaka Chaka and Brenda Fassie. She’s a mean entertainer herself, she plays the saxophone, sings, acts and dances and thinks she’d make a ‘potential’ presenter. Laveda’s favourite movies include The Notebook, Titanic and Avatar.

She entered Big Brother Hotshots to be a role model and act as a voice for Africa’s youth. Laveda says that viewers can expect ‘massive entertainment’ from her and that if she wins, she’ll give her mom some money, ‘surprise disadvantaged children’, travel and invest the rest.
Kacey Moore - Ghana
Age: 29

Born in Accra, Kacey Moore is a married poet and songwriter, with a daughter. He enjoys banku and okro stew and says his favourite books are the Bible, the dictionary, and the thesaurus! Kacey Moore also likes the music of Usher and Lauryn Hill.

Kacey Moore describes himself as a’ go-getter’, as well as ‘punctual, a leader, a creator and a voice’. His favourite quality, punctuality. It is important to him in both himself and others.

He entered Big Brother Hotshots as a business decision, seeking exposure to the rest of the world. Kacey Moore promises viewers ‘a real person with no fakeness’. If he wins the grand prize, he’ll buy houses for his wife and mother and set up a recording studio so he can record and release his own album under his own label.
JJ - Zimbabwe
Age: 23

JJ calls himself ‘an entertainer’ on the back of his work as a ‘singer, rapper, actor, songwriter and director’. His inspiration behind entering Big Brother Hotshots is the platform the show provides. ‘It’s a necessary foundation for me to be able to produce my own music even if I don’t win the money,’ he says.

He says that viewers can expect to be entertained, and that they’ll also have a gym partner every morning. If he wins the money, he’ll fix up his parents’ house, invest in his career by working n his first international album and give some money to charity.

JJ loves Italian and Japanese food, his favourite book is Shakespeare’s Macbeth and his favourite TV show is Elementary. His favourite musicians are JP Cooper, Stevie Wonder, Justin Timberlake, Kanye West and MiCasa’s J.Something. His all-time favourite films are 300, The Vow and American Gangster, with his favourite actor, Denzel Washington.

He believes that the best thing about Africa is that ‘the people are all full of life’. His favourite place in Zimbabwe is Inyaga, and outside it, Manchester in England, ‘home of the greatest football club and where I found my feet and my passion’, he says.

MH. PINDA AHUDHURI IBADA YA KUWEKWA WAKFU ASKOFU MWAIPOPO WA DAYOSISI YA SUMBAWANGA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakisalimiana na Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga (kulia) katika Ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la kiinjili la Kilutheri la mjini Sumbawanga Septemba 21, 2014. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakimkabidhi zawadi Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo (wapili kushoto) katika ibada ya kumweka wakfu Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga, Septemba 21, 2014. Kulia ni mke wa Askofu huyo, Tunsume Mwaipopo na kushoto ni Askofu Israel Mwakyolile wa Dayosisi ya Konde.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA BUNGE MAALUM LA KATIBA LEO

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba. Mhe. Samuel Sitta akiongoza bunge hilo leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Amon Mpanju akisoma Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Ezekiel Olouch akichangia mada wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Pindi Chana akichangia mada wakati wa usomaji wa Azimio la kupitisha marekebisho ya Kanuni za Bunge Maalum leo 22 Septemba, 2014 mjini Dodoma.

VIFO VYAONGEZEKA KATIKA KANISA LA TB JOSHUA LILILOPOROMOKA



Vikosi vya uokoaji vikiwa eneo lilipoporomoka jengo hilo.
 
IDADI ya watu waliofariki dunia baada ya Kanisa la Mhubiri TB Joshua kuporomoka nchini Nigeria hivi karibuni imefikia 115, huku 84 wakiwa raia wa Afrika Kusini, 7 wa Nigeria na wengine waliobaki wakiwa bado hawajafahamika wanatoka nchi gani.

Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea Kanisa hilo la 'All Nations in Lagos' lililoporomoka siku 10 zilizopita.

Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Ndege iliyobeba majeruhi 25 wa ajali hiyo imewasili mjini Pretoria ambapo wataendelea kupata matibabu.

SHIRIKA LA NYUMBA LATOA MASHINE 28 ZA KUFYATULIA MATOFALI KWA VIJANA

 Meneja wa Shirika la Nyumba mkoa wa Pwani Pauline Mrango akisoma Hotuba ya makabidhiano ya mashine 28 za kufyatulia matofali kwa vikundi vya vijana katika halmashauri zote za mkoa wa Pwani.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa pwani Pauline Mrango kwa kutoa mashine 28 za kuwasaidia vijana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali zilizotolewa na shirika la nyumba la Taifa kwenda kwenye halmashauri zote za mkoa wa Pwani
Mashine 28 zitawasaidia vijana mkoa wa Pwani kuondokana na tatizo la ajira, pili litasaidia sana katika utunzaji wa mazingira,zitasaidia wananchi kujenga nyumba za kisasa na kwa bei nafuu.

Shirika la Nyumba la Taifa limetoa mashine hizo zenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni 12 pamoja na mafunzo kwa vijana ya wiki mbili ambapo baada ya kumaliza mafunzo Shirika litatoa msaada wa shilingi laki tano kwa kila kikundi kama mtaji 

 ( Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog)

TAMASHA LA FIESTA 2014 LAACHA GUMZO MKOANI MORO




Mkali kutoka Morogoro, Stamina akiwapa burudani mashabiki wake sambamba Nay Wamitego.
Msanii wa Bongo Fleva, Afande Sele akiwapa raha mashabiki wake.
Staa wa Bongo Fleva, Mr. Blue naye ndani.
Mashabiki waliojitokeza katika Serengeti Fiesta Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.